Saturday, April 28, 2012
Thursday, April 26, 2012
WAPI USTAARABU WA MWANAMKE?
Zamani nilikuwa nahusisha kutokuwa mstaarabu inatokana na kutokuwa na elimu. Na kuwa wanawake wanaopenda kutumia lugha chafu ni wale ambao hawajasoma. Kumbe nilikuwa najidanganya; kwani siku hizi utaona matusi yanaandikwa mitandaoni mpaka unajiuliza hivi hawa wana akili timamu au wagonjwa? Kusema kweli sielewi kwanini watu tunagombana mitandaoni haswa wanawake na kuandikiana matusi ya nguoni. Tena basi wanawake haohao wanadai kuwa wao ni wasomi really? Msomi hatukani hovyo wala hana muda wa kuandika matusi mitandaoni...Tujirekebishe basi kidogo na kuacha ujinga huo!!!!!
KUNA UMUHIMU WOWOTE WA MUUNGANO?
Kila April 26 ya mwaka tunasherehekea Muungano wa Tanganyika na Zanzibar chini ya hayati JK Nyerere na Abeid Aman Karume. Hivi bado tunauhitaji au ndo wakati umefika wa kuuachia? Wenzetu wazanzibari wanalia kila siku eti wanataka kuwa huru kutoka kwa "wadanganyika" wanavyodai kuwa wananyanyasika sana! Mhh mie sielewi wananyanyasika kivipi. Is it economically, socially or politically? Na kwanini sie watu wa bara tunang'ang'ania muungano? Kuna kitu chochote cha muhimu huko visiwani ambacho tunategemea sana kiasi ambacho tukivunja muungano tutaathirika? Mimi sioni manyanyaso yoyote tunayowapa wazanzibari kama wanavyodai wao. Ninachoona ni faida kubwa tu wanapata kupitia bara.
Charles Taylor guilty of aiding S. Leone war crimes
Liberian ex-leader Charles Taylor was convicted Thursday of arming rebels during Sierra Leone's civil war in return for blood diamonds, in an historic verdict for international justice.
In the first judgement against a
former head of state by a world court since the World War II Nuremberg
trials, Taylor was found guilty of 11 counts of war crimes and crimes against humanity by the Special Court for Sierra Leone.
"The trial chamber finds you guilty of aiding and abetting of all these crimes," said presiding judge Richard Lussick.
"The chamber finds beyond
reasonable doubt that the accused is criminally responsible... for
aiding and abetting in the commission of crimes one to 11 in the
indictment," Lussick said at the court, based just outside The Hague.
Dressed in a dark suit, white
shirt and red tie, the former president stood motionless as the verdict
was read and showed no emotion afterwards.
He will be sentenced by the same court on May 30.
If sentenced to jail, Taylor will be held in a British prison.
Read more here:
Friday, April 20, 2012
RAIS ANAPOKWENDA BRAZIL KUKUTANA NA KOCHA...
Rais na mkewe wakisalimiana na na Maximo kocha wa zamani wa timu ya taifa. |
![]() | ||
Rais akisalimiana na waandishi wa habari aliowatanguliza Brazil... |
Bado sijaelewa kama ilikuwa kuna umuhimu wowote wa kwenda Brazili na kukutana na kocha wa zamani wa timu ya taifa. Na kama kuna umuhimu raisi sio kazi yake ya kwenda nje na kutafuta kocha wa timu za Tanzania. Yeye ana majukumu nyeti sana sana kuliko ya kuwa kiguu na njia kila kukicha...Tumechoka na safari zake zisizo na mpango kwa taifa..Ana wawakilishi kila nchi kwanini asiwapeleke hao? Raisi sio lazima aende kila mahali au kila shughuli wakati ana watu wa ngazi za chini ambao wanaweza kumwakilisha yeye. Kama sivyo basi hakuna haja ya kuwa na mabalozi, mawaziri lukuki nk.
Tuesday, April 17, 2012
The Secret Service Prostitution Scandal Just Keeps Getting Bigger
A preliminary investigation into the night of alleged debauchery involving members of President Obama's advance security team in Colombia has
revealed that additional military personnel may have been involved in
the prostitution scandal, Pentagon officials said Monday.
The U.S. Southern Command initially reported that five members of the U.S. special forces had participated in the partying, but preliminary reviews of hotel security tapes indicate that the number was likely much higher. A senior defense official told the AP that "at least 10 military members may have been involved."
Defense
Secretary Leon Panetta said Monday that the agency is conducting a
"full investigation" into the incident," and emphasized that he expects a
strong response.
Read more:http://articles.businessinsider.com/2012-04-16/politics/31348807_1_security-team-colombia-has-president-obama
BURUDANI-BIBI NAYE
Naona huyu bibi mwimbaji wa bongo flava alitaka aonekane kama kijana wa kisasa; akaamua kuweka haya mavazi. Waliomshauri hawakumshauri vizuri....
WAUAWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA
Wakazi
wawili wa kijiji cha Kibande wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Zegeli
Shumba (60) na mkewe Bi. Helena Zengeli(58), waliuawa na kundi la
watu wenye hasira kwa kupigwa mawe na miili yao kuchomwa moto
kutokana na imani za kishirikina.
Kamanda
Kashai amesema siku ya tukio hilo juzi majira ya saa 2.00 usiku kundi
la wananchi wa kijiji hicho waliwavamia marehemu hao kwa
kuwashambulia hadi kuwaua baada ya kutuhumiwa kuwa walikuwa
wakijihusisha na vitendo vya kichawi.
Amesema kuwa
hivi karibuni kulikua na binti mmoja kijiji hapo (hakumtaja jina)
ambaye alipotea kwa njia za kutatanisha na marehemu hao walidai kuwa
wangefanya maarifa ya kiganga kumrejesha lakini hadi wanauawa
walikuwa hawajamrejesha jambo lililoibua hasira kwa wakazi hao
MWENYEKITI UVCCM ARUSHA AJIUNGA CHADEMA

MWENYEKITI wa UVCCM, Mkoa wa
Arusha,kwa miaka mitano, James Ole Millya,ametangaza kujiuzulu nafasi
zote kuanzia Taifa hadi Mkoa na kutangaza kujiunga na Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa madai kuwa CCM imefilisika
kimawazo na haitoi matumaini kwa watanzania.
Aidha alisema hawezi
kuendelea kupanda gari lenye pancha lukuki, hivyo ameamua kupanda gari
lisilo na pancha na lenye kutoa matumaini mapya kwa watanzania.
Hayo ameyasema leo,
wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Kibo Palace,
iliyopo Jijini hapa. Amesema mara nyingi alikuwa akikemea mambo ambayo
yanaweza kubomoa chama cha CCM kwa upendo, lakini alikuwa akipuuzwa kwa
sababu ya chama hicho kuwa na kikundi cha wenyewe.
“Mimi nanukuu maneneo
ya Nyerere kuwa alishawahi kusema CCM sio mama yangu na mimi pia CCM
sio mama yangu na natangaza rasmi, kuondoka ndani ya chama hiki na
najiunga na Chadema, sababu ndicho chama chenye kuleta tumaini jipya
kwa watanzania,”alisema.
Ametaja nafasi
alizoachia ngazi ni pamoja na Mjumbe kamati ya utekelezaji UVCCM Taifa,
Mjumbe kamati ya siasa Mkoa na Mjumbe Halmashauri Kuu CCM Mkoa.
Amesema kuwa
inasikitisha kuona Vijana wa UVCCM Mkoa wa Pwani, wanatoa matamko kuwa
Rais ajaye 2015 hatatoka kanda ya Kaskazini na anayemfahamu ni Rais
peke yake ambaye ni Jakaya Kikwete.
Millya alisema cha
kusikitisha pale alipokemea kauli hiyo alipuuzwa na hadi sasa Ikulu
haijawahi kutoa kemeo kwa Vijana hao na wala kukataza kauli hizo
kutolewa, jambo lililompa jibu kuwa Ikulu inahusika kwa namna moja au
nyingine na kauli hiyo.
Aidha alisema kuna
Vijana wengi walioko ndani ya CCM wakiishi kwa matumaini ya kusubiri
kuteuliwa nafasi ya Mkuu wa Wilaya kama sio Mkoa, ila yeye hawezi
kuishi kwa matumaini kama muathirika wa Ukimwi.
Hata hivyo alitoa
wito kwa Vijana wote wenye nia ya dhati na mapenzi mema ya nchi yao,
kumfuata Chadema ambako kunatoa tumaini jipya la maisha ya watu.
Millya ambaye
alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa UVCCM tangu 2008 hadi sasa,
aliwashukuru vijana kwa kumpa ridhaa hiyo na ataendelea kuwashukuru,
ila ameamua kwa ridhaa yake kuachia ngazi zote kwa ajili ya ukombozi wa
kweli.
Millya hivi karibuni
alijitosa kinyang’anyiro cha kugombea Ubunge wa Afrika Mashari ndani ya
Chama chake cha CCM, lakini alichijiwa baharini na kutolewa jina lake.
Saturday, April 7, 2012
Tuesday, April 3, 2012
UGOMVI WA BLOGGERS
Nimemua kuzungumzia hili tatizo la bloggers kutukanana katika blogs. Najua kuwa blogs ni ya mtu binafsi lakini sio kwa kutukana watu wengine. Hili jambo linanikera sana. Imekuwa ni kawaida ya baadhi ya bloggers kutukanana/kugombana kwa mambo ya kijinga. Naita mambo ya kijinga kwasababu haiwezekani mtu kutomsifia mwingine ndio ilete ugomvi. Au kwakuwa sikutoa picha yako katika blog yangu basi ndio iwe tatizo. Mtu ameanzisha blog yake kwa hiyo ana amaamuzi ya kuandika vile anavyotaka yeye. Kama atamsifia mtu ni maamuzi yake yeye. Kwani kuna bloggers wengine ni "attention seekers" haitoshi kujiandika wenyewe wanataka na wengine nao wawe wanawaandika na kuwasifia. Wasipoandikwa basi ni matusi na kashifa zisizo na msingi... hebu tuelemike kidogo. Sio lazima jamani...kusifiwa kila siku. Tupendane na kuheshimiana kama binadamu kwani tukiwa kama bloggers sie ni kioo cha jamii.
HONGERA CHADEMA-ARUMERU MASHARIKI

Sio siri wana ARUMERU wameonyesha kuwa hawacheki na mafisadi..na wala hawababaishwi na ahadi za kijinga. Mara nyingi tumeona katika uchaguzi mbalimbali ambapo CCM huwaonga wananchi wake kwa chakula na ahadi zisizo kamilika. Ushindi wa Mh. Nassari unainyesha ushupavu wa wananchi wa kuonyesha kuchoka kuongozwa na viongozi wabovu wasiojua mwelekeo. Hawakutaka kufuata mambo ya kuongozwa na warithi; wao wanachjua ni Demokrasia ya kweli.
Kwa Mujibu wa Matokeo hayo mgombea ubunge wa Joshua
Nassari CHADEMA amepata kura 32,972, na kumshinda Mgombea mpinzani
wake mkuu katika uchaguzi huo, Sioi Sumari wa Chama cha Mapinduzi
(CCM) aliyepata kura 26,757.Kwamatokeo hayo inafanya kuwa idadi ya
Kura zilizompa ushindi Nassari wa Chadema kuwa kura 6,215 dhidi ya
Sioi Sumari CCM.
Subscribe to:
Posts (Atom)