Tuesday, April 17, 2012

WAUAWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

Wakazi wawili wa kijiji cha Kibande wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Zegeli Shumba (60) na mkewe Bi. Helena Zengeli(58), waliuawa na kundi la watu wenye hasira kwa kupigwa mawe na miili yao kuchomwa moto kutokana na imani za kishirikina.
 
Kamanda Kashai amesema siku ya tukio hilo juzi majira ya saa 2.00 usiku kundi la wananchi wa kijiji hicho waliwavamia marehemu hao kwa kuwashambulia hadi kuwaua baada ya kutuhumiwa kuwa walikuwa wakijihusisha na vitendo vya kichawi.
 
Amesema kuwa hivi karibuni kulikua na binti mmoja kijiji hapo (hakumtaja jina) ambaye alipotea kwa njia za kutatanisha na marehemu hao walidai kuwa wangefanya maarifa ya kiganga kumrejesha lakini hadi wanauawa walikuwa hawajamrejesha jambo lililoibua hasira kwa wakazi hao

No comments:

Post a Comment