Nimemua kuzungumzia hili tatizo la bloggers kutukanana katika blogs. Najua kuwa blogs ni ya mtu binafsi lakini sio kwa kutukana watu wengine. Hili jambo linanikera sana. Imekuwa ni kawaida ya baadhi ya bloggers kutukanana/kugombana kwa mambo ya kijinga. Naita mambo ya kijinga kwasababu haiwezekani mtu kutomsifia mwingine ndio ilete ugomvi. Au kwakuwa sikutoa picha yako katika blog yangu basi ndio iwe tatizo. Mtu ameanzisha blog yake kwa hiyo ana amaamuzi ya kuandika vile anavyotaka yeye. Kama atamsifia mtu ni maamuzi yake yeye. Kwani kuna bloggers wengine ni "attention seekers" haitoshi kujiandika wenyewe wanataka na wengine nao wawe wanawaandika na kuwasifia. Wasipoandikwa basi ni matusi na kashifa zisizo na msingi... hebu tuelemike kidogo. Sio lazima jamani...kusifiwa kila siku. Tupendane na kuheshimiana kama binadamu kwani tukiwa kama bloggers sie ni kioo cha jamii.
Tuesday, April 3, 2012
UGOMVI WA BLOGGERS

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment