
Sio siri wana ARUMERU wameonyesha kuwa hawacheki na mafisadi..na wala hawababaishwi na ahadi za kijinga. Mara nyingi tumeona katika uchaguzi mbalimbali ambapo CCM huwaonga wananchi wake kwa chakula na ahadi zisizo kamilika. Ushindi wa Mh. Nassari unainyesha ushupavu wa wananchi wa kuonyesha kuchoka kuongozwa na viongozi wabovu wasiojua mwelekeo. Hawakutaka kufuata mambo ya kuongozwa na warithi; wao wanachjua ni Demokrasia ya kweli.
Kwa Mujibu wa Matokeo hayo mgombea ubunge wa Joshua
Nassari CHADEMA amepata kura 32,972, na kumshinda Mgombea mpinzani
wake mkuu katika uchaguzi huo, Sioi Sumari wa Chama cha Mapinduzi
(CCM) aliyepata kura 26,757.Kwamatokeo hayo inafanya kuwa idadi ya
Kura zilizompa ushindi Nassari wa Chadema kuwa kura 6,215 dhidi ya
Sioi Sumari CCM.
No comments:
Post a Comment