 |
Rais na mkewe wakisalimiana na na Maximo kocha wa zamani wa timu ya taifa.
|
Alikuwa kapumzika kidogo tu baada ya misiba ya hapa na pale sasa huyo ameanza tena!! Kutumia fedha za wananchi kwenda nje na anachokifanya huko cha maana hakuna. Raisi wa nchi anatoka kwenda nje kukutana na kocha wa zamani wa timu ya taifa?? Au anawatanguliza waandishi wa habari (watu wake) Brazil na hao ndo waompokea huko kweli? Je hao waandishi wote wamelipiwa na makampuni yao au ni nani aliyewalipia? Ohhh nilisahau kuwa wengi wao ni wa magazeti ya serikali kwa hiyo ni pesa za serikali.
 |
Rais akisalimiana na waandishi wa habari aliowatanguliza Brazil... | | |
Bado sijaelewa kama ilikuwa kuna umuhimu wowote wa kwenda Brazili na kukutana na kocha wa zamani wa timu ya taifa. Na kama kuna umuhimu raisi sio kazi yake ya kwenda nje na kutafuta kocha wa timu za Tanzania. Yeye ana majukumu nyeti sana sana kuliko ya kuwa kiguu na njia kila kukicha...Tumechoka na safari zake zisizo na mpango kwa taifa..Ana wawakilishi kila nchi kwanini asiwapeleke hao? Raisi sio lazima aende kila mahali au kila shughuli wakati ana watu wa ngazi za chini ambao wanaweza kumwakilisha yeye. Kama sivyo basi hakuna haja ya kuwa na mabalozi, mawaziri lukuki nk.
No comments:
Post a Comment