Friday, November 16, 2012

WASANII WA KIBONGO KWA KUIGA....

Wabongo hivi hatuwezi kuanzisha kitu wenyewe bila ya kuiga? Tukiangalia MOVIES nyingi za kibongo maudhui mengi yamekaa "kinigeria" hadi kuongea kwa "kupayuka". Tujaribu basi hata kufanya vitu wenyewe basi...manake tumewaiga wazungu sana tu tukaona hapana sasa hata "wapopo" nao?
Tukija upande wa Music ndo usiseme yaani watu wana copy & paste bila hata aibu! Tushukuru kuwa nchi yetu haijulikani otherwise tungekuwa tunashtakiwa kwa mambo ya "copyright infringement". Kila siku Baraza la sanaa na wasanii wenyewe huwa wanalalamika kuwa wanaibiwa kazi  zao! Sasa na wao mbona wanaiba kazi za wenzao?

Angalia huu wimbo wa OLIVER TWIST wa D'banji  then angalia msanii LINAH wa Tanzania alivyocopy!!






Linah Oliver Twist

Thursday, November 15, 2012

UNYAMA GANI HUU KWA WATOTO WADOGO??

HAWA NDIO WANAPASWA HASA KUFUNGWA MAISHA AU KUNYONGWA KABISA. NIKIWA KAMA MWANAMKE NA MAMA; KUSEMA KWELI NALAANI VIKALI WATU AMBAO WANAWAFANYIA UKATILI WATOTO WADOGO. HII SI MARA YA KWANZA KUSIKIA MATUKIO KAMA HAYA YA WATU KUWACHOMA WATOTO MOTO. LAKINI JE WATU HAWA WANAPEWA ADHABU GANI? INATAKIWA WAPEWE ADHABU AMBAYO WENGINE WASITENDE UNYAMA HUO KABISA!!!

Mtoto huyu (3) amechomwa moto na shangazi yake ni ukatili gani huu...







































Mtoto huyu akiwa hospitali baada ya wasamaria wema; akiwa hospitali ambapo madaktari wamemfanyia upasuaji na kuondoa mkono uliothirika kwa moto!





















Mwanamke ambaye anadaiwa kumchoma moto mtoto huyo wa miaka 3. Huyu ni shangazi wa mtoto huyo kweli?? Ana rorho gani ya kuweza kufanya unyama huo??


Na Elly Mbeyale
HALI ya Mtoto Aneth Johanes (4) aliyelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kufuatia kuchomwa moto mkono wake wa kushoto na anayedaiwa kuwa ni Shangazi yake inaendelea vizuri licha ya kufanyiwa upasuaji uliolazimu kukatwa kwa mkono huo.
Kwa mujibu wa mama mdogo wa mgonjwa anayemhudumia hospitalini hapo Silvia Salvatory alithibitisha kuendelea vizuri kwa motto huyo ambapo alisema ilimlazimu kufanyiwa upasuaji kutokana na mkono huo kukosa mawasiliano na kuonekana kuvunjika.
Alisema taarifa za awali zinaonesha shangazi yake huyo Bahati Rukangara alianza kumtesa mtoto huyo muda mrefu mara baada ya kumchukua kutoka kwa wazazi wake wanaoishi Bukoba Mkoani Kagera.
Aliongeza kuwa tangu amchukue kwa wazazi wake Februari Mwaka huu amewahi kumjeruhi mkono wake wa Kulia hadi kuuvunja ambapo hadi sasa mtoto huyo alikuwa akitegemea mkono wa kushoto ambao umekatwa.
Tukio hilo la kisikitisha lilitokea juzi majira ya saa nne asubuhi baada ya majirani kusikia yowe la mtoto huyo akiomba msaada kutokana na mateso na maumivu makali aliyokuwa akiyapata kutokana na adhabu hiyo kutoka kwa Shangazi yake
Muuguzi mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya Thomas Isidori alisema hali iliyopelekea kukatwa kwa mkono wa mtoto huyo ni siri kati yake na daktari aliyemhudumia na kwamba sheria ya uuguzi inakataza kutoa taarifa ambazo ni siri.
Isidori alipoulizwa sababu za mgonjwa huyo kufanyiwa upasuaji mapema mno hadi kusababisha ulemavu alisema ni suala la kitaalamu ambalo hata yeye hawezi kulijibu na ni sheria ambayo inawataka madaktari kutunza siri za wagonjwa.
Hata hivyo muuguzi huyo alizuia kabisa waandishi wa habari kupiga picha za motto huyo baada ya kufanyiwa upasuaji huo uliosababisha kukatwa mkono kwa mgonjwa huyo.
Baadhi ya wananchi waliofika Hospitalini hapo kumjulia hali mtoto Aneth aliyelazwa Wodi namba Nane ambao hawakutaka kutaja majina yao walilaani kitendo cha madaktari kukimbilia kukata mkono mgonjwa badala ya kujaribu njia zingine za kunusuru hali hiyo.
SOURCE: sundayshomari.com


Monday, November 12, 2012

RAY C-HUJAFA HUJAUMBIKA

Ama kweli kabla hujafa hujaumbika na watu husema kuwa binadamu hujifuza kutokana na makosa. Hii inasikitisha sana, Rehema Chalamila ni mwanamziki mzuri tu lakini ona alivyoishia...hivi huku ni kulewa sifa mpaka wanatumia madawa ya kulevya au pombe? Kweli huwa wanajitakia kufikia hapo walipo? Najua sio peke yake kuna wengi tu ambao wanatumia madawa ya kulevya pamoja na vinywaji vikali ambayo baadae vinawaathiri maisha yao.

Pale umaarufu ulipokuwa juu zaidi kabla ya kuanza kutumia madawa ya kulevya.


Picha hii zinaonyesha jinsi gani madawa yalivyomuathiri..wasanii wa kibongo msaidieni mwenzenu kwani kashapata fundisho na ni fundisho kwenu nyote..Madawa si mazuri..


Wednesday, November 7, 2012

FASHION KIBONGO BONGO

Jamani kuiga sana nako si kuzuri..mtu unaiga mpaka unaonekana kichekesho! Hivi kwanini watu tunafikiria kuwa kuonyesha maungo(kuvaa half naked) ni kupendeza? Au kujikandika vipodozi usoni ni kupendeza. mhh... check out hawa "mafashonista" wa kibongo bongo.

















Sauda Mwilima umekuwa kwenye TV kwa muda mrefu sana...nadhani ungekuwa tayari umejifunza mengi. Why unajikandika vipodozi hivyo? Yaani uso na huo mkorogo umeiwa hii ni aibu!!!





















Hawa nao wakavaa sare nadhani ilikuwa kikazi zaidi haa! Hayo malemba na  pamoja na hayo mapambo ya kichwani  wanachekesha kuwema kweli!






















Mambo ya kuonyesha vivazi vya ndani tu!! kweli BONGO TAMBARARE!





















Ama kweli nilidhani kuwa tuna mitandao ambayo inaweza kutuhabarisha mambo ya urembo kwa wale wanaopenda urembo! Haswa kujua tuvae nini na wakati gani lakini hii tena mhhh! FASHION NYINGINE ZITUPITE!!! Kwani aibu tu!

Monday, November 5, 2012

Justin Timberlake, Jessica Biel Honeymoon in Tanzania!!







 


 Newlyweds Jessica Biel and Justin Timberlake can be seen getting on a private plane at the Kilimanjaro International airport in Tanzania on October 21, 2012.

 After tying the knot in an intimate, luxurious weeklong extravaganza at the Borgo Egnaza resort in southern Italy, newlyweds Justin Timberlake and Jessica Biel were ready to go wild -- really wild!
Newly released photos from Oct. 21 (two days after the wedding) reveal Timberlake, 31, and wife Biel, 30, arriving via private plane in Tanzania, on the southeastern coast of Africa. That same day, the boarded a helicopter from Kilimanjaro Airport to Singita Grumeti, a private reserve in Serengeti Park. There, the couple reportedly checked out the world famous wildlife via 4 x 4s, took a hot air balloon ride and kicked back in a luxurious lodge

Read more: http://www.usmagazine.com/celebrity-news/news/pictures-justin-timberlake-jessica-biel-honeymoon-in-tanzania-2012211#ixzz2BOik4S4F

Sunday, November 4, 2012

JOKATE!!!!!!!!!

I hope ninachookiona hapa kiwe sicho...she looks like ameanza kujichubua ngozi....Ana ngozi nzuri sana lakini kwanini ndugu zangu mnapenda kuharibu ngozi zenu!! Jirekebishe Jokate tena wewe ni msomi unatakiwa uwe mfano wa kuigwa! Sio wewe unaiga watu kuchubua ngozi!!

      

MISS TANZANIA 2012-BRIGITTE ALFRED

Huyu ndie Miss TZ 2012 Brigitte Alfred, nadhani atafanya vizuri kwenye Miss World. Au atakuwa msindikizaji kama kawaida yetu wabongo!! Tumtakie mema!

Saturday, November 3, 2012

UFUNGUZI WA MATAWI YA VYAMA VYA SIASA NJE


 Nimepokea email kutoka kwa mmoja wa watanzania anayeishi nje ya nchi yenye ujmbe ufuatao

"Wengine huenda tumeshuhudia au kusikia matawi mbalimbali ya vyama vya kisiasa  yakifunguliwa nje ya nchi yetu. Hivi tujiulize hayo matawi yanafanya nini hasa katika kuhamasisha watanzania waliopo huko?Na pia nimesikia kuwa hizi jumuiya za watanzania walipo nje nyingi ni za CCM! Na mara nyingi wanakutana kichama zaidi na si "kijamii". Ninaposema kijamii namaanisha kwa watu wote bila kujali tofauti zao za kisiasa. Pia wengine wanajifanya ni mkutano wa jumuiya za watanzania lakini ukifika kwenye mkutano ni mambo ya CCM tu!
Jamani tukumbuke kuwa kuna watanzania wengine ambao si wa CCM kuna wa vyama vingine na wengine hawafungamani na upande wowote! Kama ni mkutano wa chama semeni kuwa kutakuwa na mkutano wa CCM na sio mkutano wa jumiya ya watanzania kumbe mnaleta mambo ya kichama...
JIREKEBISHENI BASI!!!!!!!!

Mpenda maendeleo!