Saturday, November 3, 2012
UFUNGUZI WA MATAWI YA VYAMA VYA SIASA NJE
Nimepokea email kutoka kwa mmoja wa watanzania anayeishi nje ya nchi yenye ujmbe ufuatao
"Wengine huenda tumeshuhudia au kusikia matawi mbalimbali ya vyama vya kisiasa yakifunguliwa nje ya nchi yetu. Hivi tujiulize hayo matawi yanafanya nini hasa katika kuhamasisha watanzania waliopo huko?Na pia nimesikia kuwa hizi jumuiya za watanzania walipo nje nyingi ni za CCM! Na mara nyingi wanakutana kichama zaidi na si "kijamii". Ninaposema kijamii namaanisha kwa watu wote bila kujali tofauti zao za kisiasa. Pia wengine wanajifanya ni mkutano wa jumuiya za watanzania lakini ukifika kwenye mkutano ni mambo ya CCM tu!
Jamani tukumbuke kuwa kuna watanzania wengine ambao si wa CCM kuna wa vyama vingine na wengine hawafungamani na upande wowote! Kama ni mkutano wa chama semeni kuwa kutakuwa na mkutano wa CCM na sio mkutano wa jumiya ya watanzania kumbe mnaleta mambo ya kichama...
JIREKEBISHENI BASI!!!!!!!!
Mpenda maendeleo!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment