Thursday, October 27, 2011

AJALI HIZI MPAKA LINI???

Kuna usemi kuwa ajali haina kinga...lakini jamani kwa Tanzania hali inazidi kuwa mbaya. Hivi huu ni uzembe wa madereva au serikali? Mie nalaumu wote serikali, wamiliki wa vyombo vya barabarani pamoja na madereva. Nakumbuka wakati "Speed Governors" zilipoanzishwa madereva/wamiliki walikuwa wakiziweka wakijua wanafika sehemu ambayo "askari wa barabarani yupo". Sehemu ikiwa hakuna askari atakimbiza gari kupita kiasi. Licha ya hayo pia sidhani kuwa magari hufanyiwa uchunguzi (inspection) kuhakikisha kuwa hayana matatizo. Hali hii inasababisha ajali ambazo kusema kweli zingeweza kuzuiwa kama magari yangekuwa yakifanyiwa inspection. Na kama wanafanyia inspection je wanapita au ndio hongo zinatolewa ili wapitishwe? Kusema kweli inasikitisha sana...

Hivi karibuni basi la Delux Coach lilipata ajali ya kupasuka gurudumu la mbele maeneo ya Misugusugu Wilayani Kibaha mkoani Pwani Oktoba 25,2011. Gali hilo lilipinduka na kuwaka moto ambao kupoteza maisha ya baadhi ya abiria wa basi hilo  na  kuacha majeruhi .Picha za hapo chini ni za ajali  ya basi hilo ambalo liliteketekea kwa moto. Ajali kama hii na nyingine nyingi tu zinatokea kila kukicha nchini mwetu. Hivi serikali wanaona kweli au wanapuuza as usual? Pamoja na hawa madereva wetu ambao wengi wao sidhani kama wanaujuzi wowote wa kuwa barabarani.Hawajui sheria za barabarani, leseni zao wanapata baada ya kuhonga yaani ni taabu tu.




Picha zote kwa hisani ya
http://mrokim.blogspot.com/

Friday, October 21, 2011

KIKWETE AZOMEWA. NA WASOMI WA UDSM





 
RAIS Jakaya Kikwete jana amekumbana na nguvu ya wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), baada ya kupokelewa kwa mabango na nyimbo zenye ujumbe wa kuwalaani mafisadi toka kwa baadhi ya wanachuo waliokuwa wamefurika kuhudhuria maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho.
Rais Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi akiongozana na mgeni mwalikwa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, baada ya kuwasili chuoni hapo wanafunzi hao walianza kumzomea pamoja na kuonyesha mabango yaliyosomeka: ‘Miaka 50 tunalala nje’, Lectures Nkrumah makazi Bagamoyo’, ‘Miaka 50 hakuna mikopo’ ‘Tusiilipe Dowans’, ‘Mafisadi wanaiumiza nchi’ na ‘Bila juhudi zako Mwalimu Mafisadi wangetoka wapi’ na ‘Mu7 mtendee haki mpinzani wako Besgye’.
Vurugu hizo zilizodumu kwa takriban dakika 15 zilitulizwa na askari wa Kutuliza Ghasia (FFU) na wale wa jeshi la polisi waliokuwa wametanda katika eneo hilo.
Hali hiyo iliendelea hata baada ya Kikwete na mgeni wake kuingia katika ukumbi wa Nkrumah ambamo ndimo yalimokuwa yakifanyika maadhimisho hayo.
Hali ya zomea zomea ilirejea mara kadhaa Rais Kikwete alipokuwa akihutubia maadhimisho hayo hasa alipozungumzia masuala ya mikopo kwa wanafunzi.
 SOMA HAPA:
http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=35498

Saturday, October 15, 2011

BURUDANI YA LEO -KOFFI OLOMIDE (Loi)

Unakumbuka wimbo huu?Najua ulipotoka tu sehemu karibu zote za burudani ulikuwa unapigwa sana. Maharusini watu wa tarumbeta walikuwa wakiufatisha vizuri..tuburudike basi..

Thursday, October 13, 2011

MWALIMU NYERERE 1922-1999

Mwl. JK NYERERE  1922-1999

 Ikiwa ni miaka 12 tangu Raisi wa kwanza wa jamhuri ya Tanganyika na baadaye Tanzania aage dunia, watanzania bado tunamkumbuka. Alikjulikana kama mwalimu ambaye alikuwa mwalimu kweli na si wa vyeo vya kujipachika. Watanzania inatupasa tumkumbuke kwa mazuri aliyotenda; mtu wa watu aliyependa watu, mchapa kazi na mtetea  haki za wanyonge. Alitetea haki si Tanzania tu bali Afrika kwa ujumla...









Alipozungumzia kilimo au kufanya kazi kwa bidii alionyesha kwa vitendo. Kwani alikuwa akijua utawala bora ni kitu gani; na yeye kama kiongozi alikuwa mstari wa mbele kuonesha mfano.

 
Ujamaa hatukuuona umuhimu wake lakini sasa tunakumbuka yote aliyoyafanya katika kipindi chake. Tulikuwa na umeme hakukukuwa na mgao wa kijinga kama huu uliopo chini ya uongozi wa Kikwete. Alikuwa ni kiona mbali haswa kuhusu uongozi/kuchagua viongozi ndani ya CCM. Alijua  nani ni kiongozi na yupi mbabaishaji. Je hatuoni yale aliyokuwa akisema yametokea?


Aliamini kuwa maendeleo ya nchi siku zote hupatikana kwa kuwahusisha wananchi wenyewe."If real development is to take place, the people have to be involved."
Julius Kambarage Nyerere, from his book Uhuru na Maendeleo (Freedom and Development), 1973.


UTAKUMBUKWA DAIMA... REST IN PEACE.....

Saturday, October 8, 2011

Wanawake Tupendane...

 





Hivi kwanini wanawake hatupendani? Utakuta watu ni marafiki wakubwa, wanashare everything lakini  wakiwa na watu wengine wanasemana. Kuoneana wivu wa kijinga ambao hauna hata msingi. Imefikia kukuta usemi huu "mwanamke umbea kusutwa suna". Kwanini basi tusifanye mambo ya maendeleo kuliko kuchunguzana, kusemana na kugombana? Imefikia wengine wanatolena siri zao FACEBOOK na kutukanana matusi ya nguoni na huku wengine wakishangilia...Pia wanatoleana siri za ndani nikikuambia mambo yangu ujue kuwa nakuamini sasa inakuwa vipi unawaambia watu wengine? Wengine wanafikia kutishiaana kupigana! Hivi karne hii ya leo watu wanapigana kweli? Mie nadhani tushindane kwa kufanya vitu vya maendeleo.. 
 
Tena basi hao wanaotoa matusi wanadai kuwa ni wasomi, really? Wasomi hawana muda wa kuangalia mambo madogo madogo na ugomvi wa kijinga. Kama wewe ni tajiri na mwengine ni maskini haijalishi umetoa wapi utajiri wako. Kwanza matajiri hawajigambi wapo kimya na mali zao sasa sisi wakina "kapuku" kutwa maneno.

Hii tabia ni mbaya sana wanawake wenzangu tafadhali tupendane na tusitiriane jamani...
Burudika na mwanamziki Demarco "TRUE FRIEND"