RAIS Jakaya Kikwete jana amekumbana na nguvu ya wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), baada ya kupokelewa kwa mabango na nyimbo zenye ujumbe wa kuwalaani mafisadi toka kwa baadhi ya wanachuo waliokuwa wamefurika kuhudhuria maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho.
Rais Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi akiongozana na mgeni mwalikwa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, baada ya kuwasili chuoni hapo wanafunzi hao walianza kumzomea pamoja na kuonyesha mabango yaliyosomeka: ‘Miaka 50 tunalala nje’, Lectures Nkrumah makazi Bagamoyo’, ‘Miaka 50 hakuna mikopo’ ‘Tusiilipe Dowans’, ‘Mafisadi wanaiumiza nchi’ na ‘Bila juhudi zako Mwalimu Mafisadi wangetoka wapi’ na ‘Mu7 mtendee haki mpinzani wako Besgye’.
Vurugu hizo zilizodumu kwa takriban dakika 15 zilitulizwa na askari wa Kutuliza Ghasia (FFU) na wale wa jeshi la polisi waliokuwa wametanda katika eneo hilo.
Hali hiyo iliendelea hata baada ya Kikwete na mgeni wake kuingia katika ukumbi wa Nkrumah ambamo ndimo yalimokuwa yakifanyika maadhimisho hayo.
Hali ya zomea zomea ilirejea mara kadhaa Rais Kikwete alipokuwa akihutubia maadhimisho hayo hasa alipozungumzia masuala ya mikopo kwa wanafunzi.
SOMA HAPA:
http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=35498
No comments:
Post a Comment