Kuna usemi kuwa ajali haina kinga...lakini jamani kwa Tanzania hali inazidi kuwa mbaya. Hivi huu ni uzembe wa madereva au serikali? Mie nalaumu wote serikali, wamiliki wa vyombo vya barabarani pamoja na madereva. Nakumbuka wakati "Speed Governors" zilipoanzishwa madereva/wamiliki walikuwa wakiziweka wakijua wanafika sehemu ambayo "askari wa barabarani yupo". Sehemu ikiwa hakuna askari atakimbiza gari kupita kiasi. Licha ya hayo pia sidhani kuwa magari hufanyiwa uchunguzi (inspection) kuhakikisha kuwa hayana matatizo. Hali hii inasababisha ajali ambazo kusema kweli zingeweza kuzuiwa kama magari yangekuwa yakifanyiwa inspection. Na kama wanafanyia inspection je wanapita au ndio hongo zinatolewa ili wapitishwe? Kusema kweli inasikitisha sana...
Hivi karibuni basi la Delux Coach lilipata ajali ya kupasuka gurudumu la mbele maeneo ya Misugusugu Wilayani Kibaha mkoani Pwani Oktoba 25,2011. Gali hilo lilipinduka na kuwaka moto ambao kupoteza maisha ya baadhi ya abiria wa basi hilo na kuacha majeruhi .Picha za hapo chini ni za ajali ya basi hilo ambalo liliteketekea kwa moto. Ajali kama hii na nyingine nyingi tu zinatokea kila kukicha nchini mwetu. Hivi serikali wanaona kweli au wanapuuza as usual? Pamoja na hawa madereva wetu ambao wengi wao sidhani kama wanaujuzi wowote wa kuwa barabarani.Hawajui sheria za barabarani, leseni zao wanapata baada ya kuhonga yaani ni taabu tu.
Picha zote kwa hisani ya
http://mrokim.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment