Saturday, June 14, 2014
SERIKALI KWELI???? KAZI 70 WAOMBAJI 10,000!!!!
Kusema kweli inasikitisha sana kuona serikali yetu inavyodhalilisha watu... haiwezekani wanatangaza kazi na kuwakusanya watu zaidi ya 10,000 katika uwanja wa Taifa kujaza hizo kazi....
Nasema kudhalilisha kwasababu zifuatazo; kwanza kwani hawakuweza kuwaambia watu wajaze maombi mikoani mwao? kwani basi uwaambie watu wasafiri kutoka mikoani kuja Dar es Salaam kutafuta kazi. Na jinsi ninavyojua idara ya Uhamiaji ni rushwa tupu na kazi hawatoi!
Serikali imeamua kuwadhalilisha watu 10,000 au kujitoa kimasomaso ili kuonyesha kuwa inasaidia kwa kuwapa 70 positions only!!! Hapo ukweli ni kwamba tayari watu wameshapewa hizo kazi before even kutangazwa...Acheni utani jamani na muwe na aibu kidogo sio kuwanya watu wajinga kiasi hicho....ni hayo......
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment