Wednesday, August 15, 2012
TANZANIA OLYMPIC YALE YALE....Kichwa cha mwendawazimu!
Tanzania siku zote ni wasindikizaji tu kwa kitu; tunajaribu kila fani ila tunakuwa washika mkia tu. Kwenye fani ya urembo ni wa mwisho, mpira ndio usiseme yaani kwa ujumla michezo sisi ni zero! Mbona wenzetu Wakenya wanaweza? Waganda wanajaribu ila sisi tunashindwa nini? Haiwezekani unawapeleka watu walewale ambao walishindwa miaka iliyopita au ndo kujuana? Unajua kabisa mtu alichemka kipindi kilichopita then unamchukua yule yule. Mie ninahisi kuna walakini katika kuchagua wawakilishi wa mashindano ya nje "olympic". Wenzetu wanachukua miaka kujitayarisha sie tunasubiri mwezi sijui au week. halafu basi wanaondoka na "maafisa" kibao wote wa nini? Ni kupoteza tu pesa za wananchi. Ni bora kutokuwa na wawakilishi kuliko kupeleka watu ambao hawafanyi vizuri hata hawajaribu kabisa!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment