Kuna usemi kuwa Mungu si Athuman ambao unamaanisha kuwa uwezo wake haufananishwi na binadamu yoyote. Ni pale anavyoamua yeye jambo litokee linatokea lakini asipoamua yeye hakuna anayeweza kupanga wala kupangua. Je kuna mtu yeyote alidhani kuwa Dr ulimboka atatembea tena?
Mwenyekiti wa jumuia ya madaktari Tanzania Dr Steven Ulimboka aliyekuwa nchini Afrika ya kusini kwa ajili ya matibabu baada ya Kutekwa kupigwa na "watu wasiojulikana" amerejea nchini na kulakiwa na madaktari wenzake,wanaharakati wa haki za binadamu na wananchi wa kawaida. Je haki itandeka kwa wale waliomfanyia unyama kwa kufikishwa mahakamani? Au hata wakifikishwa mahakamani hukumu yao itakuwa vipi au ndio itakuwa kama kawaida yao ya "kuwaachia kwa dhamana". Au kuwa hakuna ushahidi wa kutosha au uchunguzi unaendelea...na tume imeshawekwa kufanya uchunguzi huo..
No comments:
Post a Comment