Friday, June 8, 2012
UNIFORMS ZA ATCL KWA $50,000
Hivi huku kuwaibia wananchi kutaisha lini? Yaani hawa mafisadi wanatumia kila njia ya kula pesa za wananchi. Inasemekana kuwa hizo uniforms za "cabin crews" wa shirika la ndege zimeshonwa kwa gharama ya $50,000 ambazo ni sawa na Sh.773222000 tena basi eti zimeshoneshwa nchiniChina. Kuna designers wangapi ambao wangeweza kuchona nguo hizo kwa gharama ndogo tu, Au kuna mafundi wangapi ambao wangeshona nguo hizo kwani hazina kiwango chochote cha kimataifa. Au hata kwa gharama hiyo. Ninavyoona mie material iliyotumika ni "batik" tena iliyotengenezwa cheap kabisa. Hata fundi wa mtaani kwetu angeweza kuchona tena kwa gharama ndogo sana since mshono wenyewe ni "very simple" Hii ni ugly designer ever!!!. Kweli Tanzania sasa ndo imefikia pabaya kabisa wizi wa mchana kweupe!!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment