Wednesday, June 27, 2012

Kiongozi wa mgomo wa madaktari Steven Ulimboka apigwa

Dr. Steven Ulimboka kabla ya kipigo

Hapa baada ya kupigwa.

 

Kiongozi wa mgomo wa madaktari Bw. Steven Ulimboka ameokotwa maeneo ya Mabwepande akiwa amepigwa mapanga na hali yake ikiwa ni mbaya  Fullshangwe imepata habari kuwa       kulikuwa na gari lililokuwa likipeleka katika hospitali ya TMJ Mikochezi na lilipofika hapo walimhamishia kwenye Ambulance na kumuwahisha hospitali ya Muhimbili kitengo cha mifupa Moi kwa matibabu.                                                                                                                         

Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la utekaji nyara na kujeruhi lililompata kiongozi mgomo wa Madaktari Steven Ulimboka anayedaiwa kutekwa na watu watano wakati akipata kinywaji katika klabu ya Leaders Kiondoni jijini Dar es salaam.                                                                                 

Kamanda Kova amesema Ulimboka aliokotwa na msamaria mwema ambaye hakutaka kumtaja jina lake kiusalama na kutoharibu upelelezo kuwa msamaria mwema huyo alimuokota Ulimboka katika msitu wa Mabwepande na kutoa taarifa kituo cha polisi cha Bunju, ambapo polisi aliyekuwa zamu alichukua maelezo yake na baadae Steven Ulimboka kuletwa katika hospitali ya taifa ya        Muhimbili kwa matibabu zaidi.                                                                                                       

Kamanda Kova amesema jeshi la Polisi Kanda Maalum limeunda jopo maalum kwa ajili ya uchunguzi na upelelezi wa tukio hilo la utekaji nyara, kwani ni tukio la kwanza kutoke nchini, ameongeza kwamba wahusika wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo wachukuliwa hatua za kisheria na sheria itafuata mkondo wake ili kukomesha matukio mengine kama hayo.           

SOURCE:FULL SHANGWE BLOG                                                                                             

 



No comments:

Post a Comment