![]() |
Sheikh Farid Hadi Ahmed akiongoza maandamano "ya amani". |
![]() |
Kikosi cha kutuliza fujo (FFU) kikiwa tayari kuwadhibiti waandamanaji ambao wanadaiwa kuandamana bila ya kibali |
![]() |
Kanisa ambalo linadaiwa kuchomwa na wazanzibar waliofanya maandamano. |
Maelfu ya wazanzibariwamefanya maandamano amani kuishindikiza Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar kuitisha kura ya maoni juu ya Muungano na kupeleka ujumbe kwa
Umoja wa Mataifa wa kutaka Zanzibar kujitenga kama ilivyofanya Sudan ya
Kusini.
Wazanzibari hao
wakiongozwa na Sheikh Farid Hadi Ahmed walitembea kutoka viwanja vya
Lumumba na kupitia barabara ya Kinazini, Mpigaduri, Michenzani Maskani
ya CCM Kisonge, kwa Biziredi na kurudi tena viwanja vya Lumumba.
Maandamano hayo
walioyaita matembezi ya amani yalifanyika na kuhudhuriwa na maelfu ya
wazanzibari ambapo awali kuliandaliwa kongamano kubwa lililoandaliwa na
Taasisi za Kiislamu kwa kushirikiana na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara
ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) kwa lengo la kuzungumzia mfumo wa elimu
Zanzibar.
SOMA ZAIDI:
No comments:
Post a Comment