Friday, September 30, 2011

WETU ANAWEZA KUFANYA HIVI???

 Ona Mrs.Obama; mke wa nchi yenye nguvu kuliko zote duniani alivyo "simple"! Nampenda sana huyu mama yaani hana makuu kabisa, sio kama wake wa viongozi wa nchi za kiafrika. Nazungumzia zaidi Tanzania yetu...je mke wa raisi au raisi mweyewe anaweza kwenda "shopping" Kimya kimya kama hivi au kuingia duka ambalo watu wa kawaida nao wanapata huduma? Tena basi bila hata kujulikana.....

















Hapa akiwa akiwa amemaliza "shopping" yake na anarudisha shopping cart bila ya kuwa na wasaidizi....Ingekuwa wa kwetu angefuatana na watu lukuki..Mhh tena angesafiri basi hadi US au UK kufanya shopping...na kufuja mali za umma.

Saturday, September 24, 2011

Burudani weekend hii

Burudika na Natasha Bedingfield "These Words" Have a good weekend!!

Friday, September 23, 2011

Rage Silaha nje nje

Mbunge wa Tabora Mjini,Ismail Aden Rage akiwa  amebeba  bastola kiunoni akielekea kupanda jukwaani kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Igurubi. Mheshimiwa huyu alikuwa  kwenye mkutano wa CCM wa kampeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Igunga. Sielewi alibeba  kwa ajili ya kujilinda au kutisha  watu? Kweli nchi yetu imefika pabaya yaanin viongozi wetu wanatembea silaha nje nje kabisa... Mie ninachohofia mlala hoi akimsogelea au kufanya kakosa kadogo anaweza kujeruhiwa ama kutolewa roho kabisa.
Yote heri...

Friday, September 16, 2011

NELLY KAMWELU HAKUFIKA TOP 16 !!!!!!!!!!



Nimeona blog nyingi zinampongeza Miss Universe TZ NELLY KAMWELU kwa kufika TOP 16!! Si kweli hakufika nafasi hiyo nashangaa kwanini watu wanadanganya; kama kuchemsha amechemsha kama kawaida ya watanzania kusindikiza wengine. Ila tuache kupotosha jamani na hii hapa ni list ya washindi (TOP 16) ni hawa hapa
Miss Angola Leila Lopes, Miss Ukraine Olesia Stefanka, Miss Brazil Priscila Machado, Miss Philipines Shamcey Supsup, MIss China Luo Zilin, Miss France Laury Thilleman, Miss Australia Scherri-Lee Biggs, Miss USA Alyssa Campanella, Miss Panama Sheldry Saez, Miss Costa Rica Johanna Solano, Miss Columbia Catalina Robayo, Miss Puerto Rico Viviana Ortiz, Miss Kosovo Aferdita Dreshaj , Miss Netherlands Kelly Weekers. Miss Portugal Laura Gonçalves and Miss Venezuela Vanessa Goncalves.Hakuna Tanzania hapa!!!





 Na hili nalo ni (Tanzania National Costume)? mhh! kweli jamani?