Friday, September 23, 2011

Rage Silaha nje nje

Mbunge wa Tabora Mjini,Ismail Aden Rage akiwa  amebeba  bastola kiunoni akielekea kupanda jukwaani kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Igurubi. Mheshimiwa huyu alikuwa  kwenye mkutano wa CCM wa kampeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Igunga. Sielewi alibeba  kwa ajili ya kujilinda au kutisha  watu? Kweli nchi yetu imefika pabaya yaanin viongozi wetu wanatembea silaha nje nje kabisa... Mie ninachohofia mlala hoi akimsogelea au kufanya kakosa kadogo anaweza kujeruhiwa ama kutolewa roho kabisa.
Yote heri...

No comments:

Post a Comment