WANAFUNZI WAFANYA MTIHANI UWANJANI
Hapa Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Bungo ya mkoani Morogoro akisimamia wanafunzi ambao wawalipelekwa uwanjani kufanya mtihani ili kuwaepusha "kupeana majibu".
Eti lengo ni kuwapa uhuru zaidi kwa kuwa darasani wanabanana; pia litawasaidia kupunguza tabia ya kunakili majibu kwa wale wenye mazoea hayo.
Ninavyoona mimi haya ni mateso makubwa kwa hawa watoto; hii si kufundisha. Hatuwezi kuwa na taifa bora la kesho kama tunafunza kwa kuwaumiza. Kwa nchi zilizoendelea hii ni "child abuse" na inapingwa sana. Sio kama napenda wanavyonakili majibu; ila ingetumika njia nyingine ya kuwazuia kufanya hivyo.
Picture by Dunstan Shekidele, Morogoro
No comments:
Post a Comment