Friday, July 29, 2011

Naem Gire afutiwa kesi ya Richmond




Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, jana ilimuachia huru mtuhumiwa wa kesi ya Richmond, Naeem Gire, aliyekuwa anakabiliwa na mashtaka matano ikiwemo kughushi, kutoa taarifa ya uongo na kuwasilisha hati za uongo kwa serikali baada ya ushahidi wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha makosa dhidi yake.
Naeem aliachiwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Warialwande Lema ambaye alisema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka, hakuna ushahidi ambao umeeleza jinsi mshtakiwa alitenda makosa hayo.
Alisema ili mshtakiwa aweze kusimama mahakamani na kujitetea ni wajibu wa upande wa Jamhuri kuthibitisha bila kuacha mashaka wala maswali katika ushahidi dhidi ya mtuhumiwa.
 Soma zaidi hapa:

No comments:

Post a Comment