Kusema kweli maisha ya watanzania wengi inasikitisha sana ukizingatia hakuna kiongozi wa juu ambaye anajali matatizo ya watanzania. Hivi hii tabia ya viongozi ya kuwapa watu "zawadi za muda mfupi" wanafikiria nini? Nimeshaona na kusikia mara nyingi sana kuhusu viongozi wetu wakiongozwa na Mheshimiwa wa nchi ya kuwapa watu vitu kama chakula. Tena wakati mwingine "pipi". Najua kutoa ni moyo lakini pia toa basi vitu ambavyo vitamsaidia mtu katika maisha yake.
 |
Mtoto akipewa pipi. |
Mfano mwingine ni kuwasaidia watoto mayatima/ wa mitaani kwa kuwapa mbuzi na mchele wakati wa sikukuu. Ndio nakubali unasaidia lakini ni kitu cha siku moja atakula atashiba na kusahau. Kwani basi usimpe elimu ambayo itamsaidia hapo baadaye. Tena basi atakuwa na uwezo wa kununua mwenyewe chakula.
Hii ni shule mojawapo za vijijini.. kweli mwanafunzi atakuwa nafikiria anachofundishwa hapa??
Hebu fikiria hawa wazee wa watu ambao walipigana vita vya mkoloni na kusaidia kuleta uhuru hakuna wa kuwajali. Kumbe wanakumbukwa "once a year"! Wakati wa kusherehekea siku ya mashujaa na baada yapo hakuna linaloendelea. Wanavishwa vizuri siku hiyo kama inavyoonekana "suti na viatu", mlo wa siku na waheshimiwa basi.Jamani tuwe na huruma na wazee wa watu...kama hamuwajali na kuwapa huduma kwanini mnawasumbua kuja shereheka nanyi?Tena inasemekana kuwa wengine baada ya sherehe wakaachwa na kuanza kujitafutia usafiri wenyewe wa kurudi majumbani kwao. Kama inavyoonekana hapo chini....
No comments:
Post a Comment