Saturday, July 2, 2011

JE KUTEMBEA NUSU UCHI NI UREMBO?



Tabia ya wanawake kuvaa nguo fupi au za kubana imekuwa ni kawaida katika jamii zetu. Na hii naongelea zaidi jamii ya kitanzania; ambapo wanawake wamekua wakivaa nguo fupi ambazo zinazoonyesha maungo yao kabisa. Na nyigine zinawabana sana kiasi wanashindwa hata kutembea. Swali langu ni kuwa je wanavaa ili kujisitiri, ama kupendeza? Kwa mfano mtu ni mwenye umbile kubwa (plus size) halafu ananunua nguo ambazo ni ndogo (small size) ambazo hazimtoshi kabisa.

Plus size na nguo inayofit inapendeza.
Ambapo anashindwa kutembea kutokana na udogo wa nguo hizo. Wengi wanaopenda mavazi hayo wanasema kuwa wanakwenda na wakati. Je kutembea nusu uchi ni kwenda na wakati? Na wengine wanasema kuwa mbona jamii zetu za zamani (kabla ya wakoloni) walikuwa wanatembea uchi. Na hakuna mshangao hapo hata wakivaa nguo za kuonyesha maungo yao. Lakini tunasahau kuwa enzi hizo watu walikuwa hawajajua nguo nini au wengine walikuwa hawana uwezo wa kupata mavazi. Na pia kama tutaka kuwa kama jamii za enzi zile kwanini tusivae manyasi au ngozi? Utakuta wengine ni wake za watu au mama wenye watoto; unaonyesha mfano gani kwa watoto wako na jamii kwa ujumla.  Tuache kuwa na tabia ya kusema kuwa mbona fulani wanafanya hivi basi na mimi nifanye. Kwa mfano watanzania wengi wanasema kuwa mbona wazungu wanavaa nguo fupi hamuwasemi na wengine wanatembea uchi. Kama ni hivyo tunataka kuiga kila jambo kwanini tusiige mambo ambayo ni mazuri. Mfano ni kupata elimu na kuongeza ufanisi; kuliko kufata mambo ya kijinga. Tuna uhuru lakini tusiutunie uhuru wetu vibaya...wanawake inatupasa tujiheshimu ili tuheshimiwe na jamii.Kama wewe ni mrembo utabaki kuwa ni mrembo tu hata ukivaa nguo za kuficha maungo yote,

No comments:

Post a Comment