Thursday, June 16, 2011

HALI NGUMU YA MAISHA-TANZANIA






Kila siku nakaa nikifikiria nchi yetu inaenda wapi; hasa ukiangalia maisha ya mtanzania wa kawaida. Kila kukicha shida zinaongezeka; matatizo ya umeme, afya, maji, elimu pamoja na uchumi kwa ujumla inasikitisha Kwa maoni yangu mie nawalaumu wananchi ambao wanachagua viongozi ambao wanajua kabisa kuwa hawafai. Pia hawajui kuongoza jamii nzima ya watanzania. Suala la afya kwa jamii limekuwa tatizo sugu sana; watu wanashindwa kupata matibabu mahospitalini kutokana na hali mbaya ya uchumi. Wakati viongozi wetu hawana wasiwasi kabisa wao ni safari za hapa na pale. Huduma zao za afya zinafanyika nje ya nchi; huku mwanachi aishie kijiji hajui atapata wapi hata kidonge cha dawa; au maji ya kunywa.
 Je ni nani alaumiwe? Je tumlaumu raisi wa nchi yetu au wananchi wenyewe?.

No comments:

Post a Comment