Kwanini watu wanatumia Mkorogo?
Je wanadhani kuwa uzuri ni kuwa mweupe? Tatizo hili lipo kwa wote wanawake na wanaume weusi.Inabidi watu wajivunie ngozi zao; kuna watu ambao ni weusi sana lakini wanapendeza. Kinachonisikitisha mtu anajiharibu au hajui kuwa ameharibika na kisha anajikandika vipodozi usoni. Jamani tubadilike kidogo tuacheni ulimbukeni. Sio kila mtu mweupe/mzungu kuwa ni mzuri. Madhara ya mkoro watu wanayajua sana ila tunapuuza tu; kama vile kubabuka/kuungua ngozi, kansa ya ngozi pamoja na kuwashwa. Na haya madhara yote yanasababishwa na matumizi ya chemicals kama Mercury and Hydroquinone.

Black beauty
Tujivunie rangi zetu asilia ambazo mwenyezi Mungu ametujalia.
No comments:
Post a Comment