Wednesday, October 31, 2012
MB. MUSA ZUNGU AKAMATWA KWA RUSHWA!!!!!!
Habari kutoka TBC1 zinahabarisha kuwa Mbunge wa Jimbo la Ilala, Dar es Salaam, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania, Mussa Azzan Zungu na watu wengine wanne wamekamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na rushwa katika Uchaguzi wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM unaofanyika huko Dodoma.
Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma.
Habari zaidi zinadai kuwa Zungu aliwekewa mtego na TAKUKURU na kubainika akigawa fedha alizokuwa nazo kwenye gari lake na ingawaje gari hilo lilikimbia, mawasiliano ya simu yaliyochukuliwa ni uthibitisho wa tuhuma hizo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment