Thursday, March 1, 2012

Raisi Kikwete ni"WHINE BABY"

Mheshimiwa Raisi inabidi upunguze "kulia lia" ili upate misaada; unatia aibu. Tunajua kuwa Tanzania ni nchi maskini; lakini pia kumbuka tulipata uhuru miaka hamsini iliyopita. Hakuna haja ya kuwalaumu wakoloni mpaka leo hii...huwezi kuzungumzia kuwa waliacha barabara tatu enzi zile za mwaka 47.Inakubidi wewe uchangamke na kuonyesha umefanya nini na utafanya nini katika kipindi hiki. Usiwalaumu viongozi waliopita.. Kutwa kumlaumu Nyerere kwanini usikubali tu kuwa umeshindwa kuongoza?
 Hii  sasa ni awamu yako..' punguza longolongo, kuonyeshea watu vidole na ufanye kazi kutimiza uliyoahidi.
Kazi ya raisi si kuongea kwa maneno ni vitendo ndivyo vitaonyesha wewe ni kiongozi wa aina gani...

No comments:

Post a Comment