KUMBUKUMBU ZA MWAKA 2011
Haya ni baadhi ya matukio ambayo yalitokea mwaka 2011. Mengi yametokea kutokana na uzembe wa serikali yetu ya kutojali wanachi wake.Nikianzia na ajali ya Meli ya MV ISLANDERS ambayo watu waliopetza maisha yao; wengi wao wakiwa ni watoto wadogo. Serikali imeshindwa kutoa idadi kamili ya waliopoteza maisha; na hata waliosababisha uzembe huo nao wameachiwa. kama kawaida "TUME" iliiundwa kuchunguza....
Mafuriko yalitokea jijini Dar es Salaam ambayo yamesababisha maafa makubwa hasa kwa watu wanaoishi mabondeni. Idadi ya waliopoteza maisha (?), kusema kweli waseme tu haijulikani. Kama watu wamejenga bila vibali je watajua wangapi wamepoteza maisha? Mwenyezi Mungu awalaze pema peponi wote..
Mabomu ya GONGOLAMBOTO yalisababisha maafa ya watu na uharibifu wa wali za wananchi. Idadi ya waliopoteza maisha kama kawaida ina utata; kwani serikali haikutoa idadi kamili.
Maandamano ya CHADEMA ambayo ni kuupinga uongozi wa CCM yaliambatana na vurugu ambazo zilisababisha kifo, uharibifu wa mali pamoja na majeruhi.
MIGOMO ya wanafunzi kudai posho zao; ambazo pia ziliandamana na machafuko.
MAANDAMANO ya wafanyabishara wadogo sehemu mbalimbali nchini...ikiwemo Mkoani mwanza na Mbeya.Ambapo serikali ilitumia vyombo vya dola kuwadhibiti wafanyabishara hao.
No comments:
Post a Comment