Tuesday, January 31, 2012

KIKWETE KUWA NA UTU KIDOGO...

Najua kuzungumzia huruma hii inajulikana wazi kuwa KIKWETE NA BARAZA LAKE hawana huruma kabisa na wananchi wao! Haiwezekani watu umeme mmewakatia, huduma za jamii ni mbaya kuliko. Huduma ya afya ndo usiseme...madaktari wetu wanajitahidi hivyo hivyo. Kumbe wanapewa posho ya 10,000 kweli? wakati wabunge wanajilalia tu bungeni wanapewa 350,000 kwa nini lakini? Haiwezekani kabisa na inasikitisha sana madktari wanafanya kazi kubwa kuliko hao wanaoenda kukoroma bungeni..for real wanafanya kitu gani cha maana...Kwa mtu ambaye ana utu na kufikiria wanadamu wenzake wanaokufa kwa kukosa huduma za afya hospitalini; asingewaongeza wabunge posho. Instead, angewapa madaktari japo kidogo ili warudi kutoa huduma. Tumnajua kuwa hamjali kwa kuwa nyie wenzetu mkijikwaa kidogo mnapanda ndege kwenda nje ya nchi kutibiwa. Ila sisi watoto wa maskini hata Muhimbili kulipaa fees za kumuona huyo daktari shida.... Kwa mtu mwenye akili timamu angepima lipi lina uzito kuwapa posho wakaa bure au kuwaongeza wachapa kazi wanaokoa maisha ya wanyonge...
KIKWETE NA BARAZA LAKE HAWANA UTU...

Tuesday, January 3, 2012

MADAKTARI MUHIMBILI WAGOMA

Madaktari 229 wagoma Muhimbili  
Zacharia Osanga
MADAKTARI 229 walioko katika mafunzo kwa njia ya vitendo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam, wamegoma wakishinikiza kulipwa jumla ya Sh176 milioni, zikiwa ni posho zao za kijikimu.Mgomo huo ulianza jana mchana na madaktari hao wamesema hautakwisha hadi hapo watakapolipwa fedha zao.

Madaktari hao ni wa kada za tiba ya vinywa, maabara, dawa na wafamasia ambao wametishia mgomo huo utaenea hadi katika Hospitali za Mnazi Mmoja, Zanzibar, Bombo mkoani Tanga, Temeke, Amana na Mount Meru, jijini  Arusha ambako wenzao nao hawajalipwa kwa miezi miwili.

Wakizungumza  mbele ya Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Deo Mtasiwa. aliyekwenda Muhimbili kuwasikiliza madai yao,  madakatari hao walisema maisha yao yamekuwa magumu kwa sababu ya kukosa fedha za kujikimu.
 Mmoja wa wataalamu hao,  Dk Frank Kagoro, alisema  tatizo  lililopo ni kukosekana kwa uwajibikaji kwa upande wa Serikali.

“Mnachukulia mambo kirahisi sana tupo katika mafunzo lakini tutawezaje kufanya kazi bila fedha. Tunajua tuna wagonjwa na wanaumia kwa sababu ya hatua hii, hivi nani hapa asiyejua kuwa muda huu alitakiwa kuwa wodini akiwapitia wagonjwa, hivi kweli mnatupa kipaumbele," alihoji Dk Kagoro.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa madaktari hao, Dk Mally Deogratius, alisema madai yao ni zaidi ya Sh176 milioni, zikiwa ni posho za kati ya Novemba na Desemba mwaka jana, kipindi ambacho hawakulipwa.
Hata hivyo, Dk Mtasiwa aliwahakikishia kuwa malipo yao yatafanyika leo na kwamba yamechelewa kutokana na taratibu za Serikali katika malipo.
http://www.mwananchi.co.tz/news/4-habari-za-kitaifa/19018-madaktari-229-wagoma-muhimbili.html
KUMBUKUMBU ZA MWAKA 2011
Haya ni baadhi ya matukio ambayo yalitokea mwaka 2011. Mengi yametokea kutokana na uzembe wa serikali yetu ya kutojali wanachi wake.

Nikianzia na ajali ya Meli ya MV ISLANDERS ambayo watu waliopetza maisha yao; wengi wao wakiwa ni watoto wadogo. Serikali imeshindwa kutoa idadi kamili  ya  waliopoteza maisha; na hata waliosababisha uzembe huo nao wameachiwa. kama kawaida "TUME" iliiundwa kuchunguza....



Mafuriko yalitokea jijini Dar es Salaam ambayo yamesababisha maafa makubwa hasa kwa watu wanaoishi mabondeni. Idadi ya waliopoteza maisha (?), kusema kweli waseme tu haijulikani. Kama watu wamejenga bila vibali je watajua wangapi wamepoteza maisha? Mwenyezi Mungu awalaze pema peponi wote..



Mabomu ya GONGOLAMBOTO  yalisababisha maafa ya watu na uharibifu wa wali za wananchi. Idadi ya waliopoteza maisha kama kawaida ina utata; kwani serikali haikutoa idadi kamili.





Maandamano ya CHADEMA ambayo ni kuupinga uongozi wa CCM yaliambatana na vurugu ambazo zilisababisha kifo, uharibifu wa  mali pamoja na majeruhi.





 MIGOMO ya wanafunzi kudai posho zao; ambazo pia ziliandamana na machafuko.
 MAANDAMANO ya wafanyabishara wadogo sehemu mbalimbali nchini...ikiwemo Mkoani mwanza na Mbeya.Ambapo  serikali ilitumia vyombo vya dola kuwadhibiti wafanyabishara hao.