Hivi karibuni migomo mbalimbali inatokea nchini kupinga mwenendo wa serikali yetu. Hii inaonyesha wazi kuwa serikali imeshindwa aidha kutekeleza ahadi walitoa kwa wananchi anu ni dharau wanaonyesha juu ya wapiga kura wao. Inasikitisha kuona kuwa nchi yetu inaenda pabaya; na viongozi wamekaa kimya. Kama matukio ya hivi karibuni huko mbeya ambapo wafanyabishara waligoma. Hii ni kupinga serikali au kutoridhika na uongozi wa Raisi Kikwete. Badala ya kuwasaidia kutatua matatizo yao ndio kwanza wanatumia nguvu ya vyombo vya dola. Huwezi kuwahamisha watu bila kuwaambia wapi waende lakini si unajua tena viongozi wetu wao ndio kila kitu. Sawa huwenda wakawa wanavunja sheria ya kupanga biashara zao barabarani lakini inabidi waonyeshwe sehemu ya kwenda kabla ya kuwatimu. Tena basi si ndi nye mnaosema kuwa watu wajiajiri? Mnataka waende wapi anu wafanye nini sasa? Wawe vibaka?
Wafanyabishara wa mjini Mbeya waligoma kutoka na kuhamishwa kwenye maeneo wanayofanyia biashara zao. Magari yalichomwa moto na barabara kufungwa.Fujo hizi pia zilitokea huko Mwanza ambapo pia wafanyabiashara ndogondogo waligoma.
Sio wafanyabishara tu ambao hawaridhiki na utendaji wa serikali yetu hata wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali hawaridhiki na ahadi zisizokamilishwa na serikali. Pichani juu ni wanafunzi kutoka chuo cha IFM ambao nao waligoma.
Hawa nao ni wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) ambao pia waligoma. Inaonekana wazi kuwa serikali hairidhishi utendaji wake kwa wananchi kawa walivyoahidi.
No comments:
Post a Comment