Watoto wetu wakihangaika kupata usafiri wa kuwapeleka shule.Imeshakuwa ni kawaida kwa wanafunzi kunyanyasika katika daladala.
Inapotokea msamaria mwema anapowaonea huruma watoto hawa hawachagui ni bora kufika shule.
Je lini nasi tutafikia hali hii? Japo kuwa na mabasi machache ya kuwafikisha watoto wetu mashuleni. Nakumbuka tulikuwa na school buses ambazo zilisaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa tatizo la usafiri kwa wanafunzi. Lakini baada ya muda mfupi mabasi yote yakapotea na hali inazidi kuwa mbaya. Ni watu wachache waliofaidika na mradi ule wa school buses na hii ni kutokana na rushwa iliyokithiri nchini kwetu.
No comments:
Post a Comment