Friday, August 12, 2011

AMBULANCES ZA KIBONGO

Sijui niite ni magari au pikipiki za miguu mitatu ila ndio yanategemewa kutumika kuwasafirisha wagonjwa(ambulance). Ninachojiuliza yatapita njia gani? Na je yatakuwa yakitumia barabara pamoja na magari mengine ambayo mjini Dar ni kama utitiri. Hii inaonyesha wazi serikali yetu haipo serious na maisha ya wananchi wake. Madereva wetu wenyewe hawana ujuzi barabarani sasa wakipewa "hizo pikipiki" na wagonjwa wake watafika salama kweli?

Mhh!hapa kweli mgonjwa atapona au ndo njia ya kumuongezea "ugonjwa" mwingine.Haipendezi viongozi kutumia magari ya fahari yanayonunuliwa kwa mamilioni ya kodi za wananchi, wakati wananchi wanateseka. Eti wasafirishwe kwa  ambulance za bajaji, pikipiki ambazo sio salama kwa maisha yao. Hivi ni lini watatusikia kilio chetu?


No comments:

Post a Comment