Monday, August 29, 2011
Wednesday, August 24, 2011
ONA WANAJESHI WETU WANAVYOADHIRIKA...
Haya ni maoni ya msomaji mmoja ambaye amejitambulisha kuwa ni mwanajeshi. Nimeyapata kutoka katika Gazeti la RAIA MWEMA. Maoni haya yaliwekwa katika thread isiyohusika; ila nimeiona kuwa ni muhimu sana. Hii nini aibu kwa serikali yetu; inaonesha kuwa ambavyo haijali watu wake. Si vizuri kuwapeleka watu kwenye hatari na huku mkiwanyonya maslahi yao. Inaonesha kama mmewatoa sadaka vile..
Source: http://raiamwema.co.tz/spika-makinda-aja-na-mpya-dodoma
WABUNGE NIKWELI KWA SASA
WABUNGE NIKWELI KWA SASA WAMEANZA KUTIMIZA WAJIBU WAO TUNAOMBA NA HILI LA JESHI LA ULINZI WALIZUNGUMZIE WASIOGOPE MAANA BAADAYE ITAKUWA HATARI HASA HUYU SWAHIBA WA RAIS JK KIKWETE LT GENERAL ABDALAHAMAN SHIMBO AMEKUTWA KWENYE ACCOUNT YAKE YA NJE IKIWA NAKIASI CHA TRION 3…. NA UKI MFUATILIA HANA MIRADI YA KUMWEZESHA KUMILIKI KIASI KIKUBWA CHA FEDHA HIZO, NA WAKATI HUOHUO ASKARI WA KULINDA AMANI LEBANON/DAR-FUU WAMEKUWA WAKI LALAMIKA KWENYE VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUFANYIWA UFISADI NA GENERAL HUYO; POSHO ZAO ZA CHAKULA ZINA INGIZWA KWEYE ACCOUNT YAKE, PIA WANALIINGIZIA TAIFA USD 5000 KWA KILA ASKARI CHA AJABU YEYE ANA WALIPA USD 823 BADALA YA USD 2000 SASA HUONI KAMA HUO NIUFISADI? AJABU WALINZI WA AMANI LEBANON/DAR-FU SUDANI, HATUJALIPWA POSHO ZETU, YAPATA SASA MIEZI MINANE (8) KIKUBWA HATA SABUNI YA KUOGEA, KUFULIA TUMEANZA KUKOPA KWA WENYEJI KITU AMBACHO NI AIBU HATUNA JINSI. ZIPO PESA ZILIZOTOLEWA NA RAIS WA KOMORO KWA WANAJESHI WOTE WA TANZANIA KAMA ASANTE BAADA YA KUMUONDOA KANALI BAKARI. AJABU PESA HIYO HATUJALIPWA, HUWENDA NAYO IMEINGIZWA KATIKA ACOUNT YA NJE YA HUYO FISADI. SISI ASKARI TUMEKUWA WAZALENDO KWA MDA MLEFU LAKINI SASA TUMEFIKA PAHALA TUNASHINDWA, NA HATAHIVYO TUPO TAYARI KUWAUNGA MKONO WAPINZANI NA WATANZANIA WOTE WAKIWA TAYARI KUFANYA MAANDAMANO YA NCHI NZIMA KUPINGA SERIKALI ILIYOPO MADARAKANI KAMA YALE YALIYOFANYIKA MISRI YA KUSINIKIZA UTAWALA ULIOPO MADARAKANI UONDOKE BAADA YA KUSHINDWA KUTEKELEZA MAJUKU YAKE. (KAPO KAKIKUNDI KADOGO NDANI YA JESHI KALIKOPEWA MAMLAKA MAZITO YA KURIPOTI MABAYA NA MAZURI KUMBE NI KAKINDI KA KUPTOSHA UKWELI WA MAMBO YANAYOTENDWA NDANI YA JESHI LETU, BADALA YAKE HURIPOTI TAARIFA ZA UONGO KUWA HALI YA JESHI KIUSALAMA NI SHWARI, UTAWALA NA VIFAA NI SALAMA LAKINI SI KWELI KUNA MOSHI UNAFUKA CHINI IPO SIKU MOTO UTAWAKA)Source: http://raiamwema.co.tz/spika-makinda-aja-na-mpya-dodoma
Tuesday, August 23, 2011
Libya Rebels Seize Qaddafi Compound in Fight for Tripoli
Libyan rebels seized control of Muammar Qaddafi’s compound in Tripoli, capturing weapons and documents, as one of their leaders sought to avert a wave of retribution against former regime supporters.
Mahmoud Jebril, a member of the National Transitional Council, called on Libyans to unite and build a “modern nation” without acting on their own to settle scores.
“After the transition and elections, people who suffered injustices will regain their rights,” he said at a press conference in Doha, Qatar.
Rebels broadened their hunt the elusive Qaddafi as fighting against regime loyalists flared elsewhere, including around the southern city of Sabha, rebel officials said. Sabha is a regime stronghold that is home to a major military base.
“As long as Qaddafi remains in Libya, then there will be no security,” Abdel Hafiz Ghoga, vice president of the rebel National Transitional Council, said in a telephone interview from Benghazi. “He must be finished off, either through death or capture.”
Oil advanced for a second day amid signs that a recovery in Libyan crude production may take longer than expected. Output from Libya, which has the largest proven reserves of any African country, dropped to 100,000 barrels a day in July, down from the 1.6 million barrels pumped before the uprising started.
Wednesday, August 17, 2011
Wanaokula hadharani, kuvaa nguo fupi Zanzibar kukiona
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imelitaka Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaokula hadharani na kuvaa nguofupi wakati huu wa mfungo mtukufu wa Ramadhani.
Tamko hilo limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed, alipozungumza na waandishi wa habari jana.
Alisema serikali imeamua kutoa agizo hilo baada ya kujitokeza baadhi ya watu kuonekana wakila mchana hadharani na baadhi ya vijana kuonekana wakiwa wamelewa na kuranda mitaani kinyume na misingi ya mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Aidha, alisema baadhi ya wanawake wamekuwa wakionekana mitaani wakiwa wamevaa nguo zisizokuwa na heshima.
Waziri Aboud amesema kwamba baadhi ya migahawa na nyumba za kulala wageni zimekuwa zikitoa huduma mchana katika kipindi cha Mwezi Mtukufu. Waziri Aboud alisema kimsingi wananchi hawazuiwi kula mchana kulingana na imani zao, lakini wanatakiwa kufanya hivyo wakiwa katika maeneo ya faragha kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.
“Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inawataka wale wote wanaojishirikisha na vitendo hivyo waache mara moja kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria pamoja na kwenda kinyume na amri ya Mwenyezi Mungu na mafundisho yake Mtume Mohammad,” alisema.
Aidha, alisema serikali inatarajia wananchi wote Unguja na Pemba watashirikiana kurudisha heshima ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.
Waziri Aboud amesema serikali imeamua kutoa tamko hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka Jumuiya moja ya kidini Zanzibar juu ya kuwepo watu wanaokula mchana na kuvaa nguo fupi bila kuzingatia misingi ya mfungo wa Mwezi wa Ramadhani.
SOURCE: NIPASHE
Subscribe to:
Posts (Atom)