Mr President Unatusikia lakini???
Tangu alipoingia madarakani Mheshiwa Rais umekuwa kama vile husikii vilio vyetu sisi wananchi. Tatizo la umeme limekuwa sugu watu wameshalalamika sana lakini hakuna la maana ambalo limefanywa ili kutatua tatizo hili. Biashara za watu zinadoda kutokana na ukosefu wa umeme; Ingawa kuna watu ambao wanatumia majenereta ila ni wachache. Si kila mtu anaweza kumudu jenereta kwanza ni gharama; pamoja na bei za mafuta zipi juu sana kwa mtu wa kipato cha kawaida. Watu tumechoka kutumia vibatari na mishumaa. Shida ya maji pia imekuwa ni tatizo sugu tanzania. Na hili pia linasababishwa na kukosekana kwa umeme.Kama jiji la Dar es salaam watu wanategemea maji kutoka kwenye visima vya watu binafsi ambao wanatumia umeme kusukuma maji hayo.
![]() |
Msichana akichota maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani. |
Tusizungumzie mijini na huko vijijini hali ya wananchi ni mbaya sana; watu wnakunywa maji ambayo si salama kabisa kwa afya zao. Maji hayo wanayapata kutoka katika madimbwi yaliyosimama; ambayo yatumiwa na wanyama pamoja na binadamu. Hii inasbabisha kupata magonjwa kama kichocho kipindu pindu na mengine ambayo yakuambukiza.
Serikali inasema watu tujiajiri kutokana na kuwa ajira ni shida; sawa mie mtoto wa mlalahoi nimejitahidi kufanya angalau biashara ndogondogo. Lakini mbona mnawatuma mgambo wa jiji kunyang'anya mali na kuwapiga wafanyabishara. Mie nadhani hii ndio kujiari huku ama? Mnataka watu wafanye nini? Waende kuiba? Watu wanasoma lakini kazi hawapati; kwani ukienda kutafuta kazi lazima utoe kitu kidogo ili uipate hiyo kazi.
Wafanyabiashara wa jiji la Mwanza wakidhibitiwa na askari baada ya kupinga kuhamishwa kwa nguvu kutoka eneo wanalofanyia biashara.(picha na Michuzi) |
Sio siri inasiitisha sana kuona watu wanaishi maisha ya shida kutokana na bei ya vitu kuwa juu sana. Wafanyabiashara wanapandisha bei ya vyakula wanavyotaka wao; hivi mamlaka inayoshughulika na mambo ya chakula inafanya nini?
Huduma za afya zinasikitisha haiwezekani wagonjwa watatu kulala kitanda kimoja kweli? Hospitalini huduma ni mbaya, hakuna madawa kwa wagonjwa; na rushwa imeenea na hakuna mtu wa kugalia hilo.
Mojawapo ya Chumba cha wazazi katika hospitali zetu. |
Wagonjwa wengine wanalala chini kutokana na ukosefu wa vitanda. Hatjui kuwa hii inasababisha kuenea kwa magonjwa mengine.
Kila kukicha watu wanagoma kuonyesha kutoridhika na serikali laki hawasikilizwi ndio kwanza wanapigwa mabomu. Demokrasia ipo wapi? Serikali kutumia nguvu kwa wanachi wake kwa kweli inasikitisha sana; huo si ubinadamu huo.
Mungu ibariki Tanzania.
No comments:
Post a Comment