Friday, May 4, 2012

Dr Mwakyembe roho nyeupe...unafiki mtupu!!!


 Naona sasa Dr. Mwakyembe roho nyeupe baada ya kuzawadiwa "ulaji" na mkuu wa ulaji au mkuu wa kaya. Kuteuliwa kwa Mwakyembe kuwa waziri wa uchukuzi naona ni njia mojawapo ya kumshukuru kwa kumfichia siri mkuu wa kaya. Nakumbuka alikuwa anaahidi kufichua siri kila kukicha lakini ghafla alikaa kimya. Mhh kumbe alikuwa anasubiria akijua atapatiwa something na mkuu wa kaya. Huu ni unafiki mtupu wa viongozi wetu kucha ni kufichiana maovu na kutufanya sisi wananchi wapumbavu.Kwahiyo inaonyesha kabisa yale yote aliyokuwa akiyasema yalikuwa ni dangya toto. Na kuwa yeye na wengine wote aliokuwa akiwashutumu ni walewale. Wote wapo pamoja katika kula pesa za watanganyika.

KWELI ANA MENGI YA KUJIFUNZA



Hivi SHY ROSE alishindwa kutengeneza keki isiyo na rangi zinazohusiana na chama chake? Wakati anajua kabisa anakwenda shrehekea na watu wanaotofautiana kiitikadi. Pichani Mbunge wa CHADEMA Halima Mdee akiikataa keki hiyo...
Picha na Mroki Mroki

Saturday, April 28, 2012

BURUDANI YA LEO-DUNIA TUNAPITA

Tuburudike na Samba Mapangala dunia tunapita...

Thursday, April 26, 2012

WAPI USTAARABU WA MWANAMKE?

 

Zamani nilikuwa nahusisha kutokuwa mstaarabu inatokana na kutokuwa na elimu. Na kuwa wanawake wanaopenda kutumia lugha chafu ni wale ambao hawajasoma. Kumbe nilikuwa najidanganya; kwani siku hizi utaona matusi yanaandikwa mitandaoni mpaka unajiuliza hivi hawa wana akili timamu au wagonjwa? Kusema kweli sielewi kwanini watu tunagombana mitandaoni haswa wanawake na kuandikiana matusi ya nguoni. Tena basi wanawake haohao wanadai kuwa wao ni wasomi really? Msomi hatukani hovyo wala hana muda wa kuandika matusi mitandaoni...Tujirekebishe basi kidogo na kuacha ujinga huo!!!!!

KUNA UMUHIMU WOWOTE WA MUUNGANO?


 Kila April 26 ya mwaka tunasherehekea Muungano wa Tanganyika na Zanzibar chini ya hayati JK Nyerere na Abeid Aman Karume. Hivi bado tunauhitaji au ndo wakati umefika wa kuuachia? Wenzetu wazanzibari wanalia kila siku eti wanataka kuwa huru kutoka kwa "wadanganyika" wanavyodai kuwa wananyanyasika sana! Mhh mie sielewi wananyanyasika kivipi. Is it economically, socially or politically? Na kwanini sie watu wa bara tunang'ang'ania muungano? Kuna kitu chochote cha muhimu huko visiwani ambacho tunategemea sana kiasi ambacho tukivunja muungano tutaathirika? Mimi sioni manyanyaso yoyote tunayowapa wazanzibari kama wanavyodai wao. Ninachoona ni faida kubwa tu wanapata kupitia bara.