Tuesday, April 17, 2012

MWENYEKITI UVCCM ARUSHA AJIUNGA CHADEMA








MWENYEKITI wa UVCCM, Mkoa wa Arusha,kwa miaka mitano, James Ole Millya,ametangaza kujiuzulu nafasi zote kuanzia Taifa hadi Mkoa na kutangaza kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa madai kuwa CCM imefilisika kimawazo na haitoi matumaini kwa watanzania.

Aidha alisema hawezi kuendelea kupanda gari lenye pancha lukuki, hivyo ameamua kupanda gari lisilo na pancha na lenye kutoa matumaini mapya kwa watanzania.

Hayo ameyasema leo, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Kibo Palace, iliyopo Jijini hapa. Amesema mara nyingi alikuwa akikemea mambo ambayo yanaweza kubomoa chama cha CCM kwa upendo, lakini alikuwa akipuuzwa kwa sababu ya chama hicho kuwa na kikundi cha wenyewe.

“Mimi nanukuu maneneo ya Nyerere kuwa alishawahi kusema CCM sio mama yangu na mimi pia CCM sio mama yangu na natangaza rasmi, kuondoka ndani ya chama hiki na najiunga na Chadema, sababu ndicho chama chenye kuleta tumaini jipya kwa watanzania,”alisema.

Ametaja nafasi alizoachia ngazi ni pamoja na Mjumbe kamati ya utekelezaji UVCCM Taifa, Mjumbe kamati ya siasa Mkoa na Mjumbe Halmashauri Kuu CCM Mkoa.

Amesema kuwa inasikitisha kuona Vijana wa UVCCM Mkoa wa Pwani, wanatoa matamko kuwa Rais ajaye 2015 hatatoka kanda ya Kaskazini na anayemfahamu ni Rais peke yake ambaye ni Jakaya Kikwete.
Millya alisema cha kusikitisha pale alipokemea kauli hiyo alipuuzwa na hadi sasa Ikulu haijawahi kutoa kemeo kwa Vijana hao na wala kukataza kauli hizo kutolewa, jambo lililompa jibu kuwa Ikulu inahusika kwa namna moja au nyingine na kauli hiyo.

Aidha alisema kuna Vijana wengi walioko ndani ya CCM wakiishi kwa  matumaini ya kusubiri kuteuliwa nafasi ya Mkuu wa Wilaya kama sio Mkoa, ila yeye hawezi kuishi kwa matumaini kama muathirika wa Ukimwi.
Hata hivyo alitoa wito kwa Vijana wote wenye nia ya dhati na mapenzi mema ya nchi yao, kumfuata Chadema ambako kunatoa tumaini jipya la maisha ya watu.

Millya ambaye alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa UVCCM tangu 2008 hadi sasa, aliwashukuru vijana  kwa kumpa ridhaa hiyo na ataendelea kuwashukuru, ila ameamua kwa ridhaa yake kuachia ngazi zote kwa ajili ya ukombozi wa kweli.
Millya hivi karibuni alijitosa kinyang’anyiro cha kugombea Ubunge wa Afrika Mashari ndani ya Chama chake cha CCM, lakini alichijiwa baharini na kutolewa jina lake.

Saturday, April 7, 2012

Tuesday, April 3, 2012

KWELI AKILI NI NYWELE....


UGOMVI WA BLOGGERS


 


 Nimemua kuzungumzia  hili tatizo la bloggers kutukanana katika blogs. Najua kuwa blogs ni ya mtu binafsi lakini sio kwa kutukana watu wengine. Hili jambo  linanikera sana. Imekuwa ni kawaida ya baadhi ya bloggers kutukanana/kugombana kwa mambo ya kijinga. Naita mambo ya kijinga kwasababu haiwezekani mtu kutomsifia mwingine ndio ilete ugomvi. Au kwakuwa sikutoa picha yako katika blog yangu basi ndio iwe tatizo. Mtu ameanzisha blog yake kwa hiyo ana amaamuzi ya kuandika vile anavyotaka yeye. Kama atamsifia mtu ni maamuzi yake yeye. Kwani kuna bloggers wengine ni "attention seekers" haitoshi kujiandika wenyewe wanataka na wengine nao wawe wanawaandika na kuwasifia. Wasipoandikwa basi ni matusi na kashifa zisizo na msingi... hebu tuelemike kidogo. Sio lazima jamani...kusifiwa kila siku. Tupendane  na kuheshimiana kama binadamu kwani tukiwa kama bloggers sie ni kioo cha jamii.

HONGERA CHADEMA-ARUMERU MASHARIKI



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEitDLon5DSCr-7O0PbGQ4YvAr4MM1taZaSYdkt1fRERPelDw4mt5_UmmmZt89R1swWqEQK-jX3WPfTzYUQAvAlYIGFYiVRHrnrv2hQYETJ-lcoblLtTYZvRbr-987rjm6n78txeqbvKqLyR/s640/the+two.jpg

Bw. Joshua Nassari wa CHADEMA


Sio siri wana ARUMERU wameonyesha kuwa hawacheki na mafisadi..na wala hawababaishwi na ahadi za kijinga. Mara nyingi tumeona katika uchaguzi mbalimbali ambapo CCM huwaonga wananchi wake kwa chakula na ahadi zisizo kamilika. Ushindi wa Mh. Nassari unainyesha ushupavu wa wananchi wa kuonyesha kuchoka kuongozwa na viongozi wabovu wasiojua mwelekeo. Hawakutaka kufuata mambo ya kuongozwa na warithi; wao wanachjua ni Demokrasia ya kweli.
Kwa Mujibu wa Matokeo hayo mgombea ubunge wa Joshua Nassari CHADEMA amepata kura 32,972, na kumshinda Mgombea mpinzani wake mkuu katika uchaguzi huo, Sioi Sumari wa Chama cha Mapinduzi (CCM) aliyepata kura 26,757.Kwamatokeo hayo inafanya kuwa idadi ya Kura zilizompa ushindi Nassari wa Chadema kuwa kura 6,215 dhidi ya Sioi Sumari CCM.